HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 16, 2015

MAKALA YA SHERIA: NAMNA YA KUMSAIDIA NDUGU YAKO KUPATA DHAMANA POLISI


1.DHAMANA NININI.

Dhamana ni hatua ambapo mtu ambaye tayari ni mtuhumiwa wa kosa fulani huachiwa huru kwa muda ili kusubiri hatua za kufikishwa mahakamani au kama tayari amefikishwa mahakamani husubiri kuendelea kwa kesi yake. Kwahiyo ili lije suala la dhamana ni lazima uwe umetuhumiwa polisi au tayari umefikishwa mahakamani. Ieleweke kuwa kuna aina kuu mbili za dhamana. Kwanza dhamana ya polisi na pili dhamana ya mahakamani.Hapa tunazungumzia dhamana ya polisi.

2.UKIOMBWA HELA KWA AJILI YA DHAMANA KATAA.

Dhamana hutolewa bure. Ieleweke wazi kuwa hakuna malipo yoyote yanayotakiwa kutolewa ili mtuhumiwa au mshtakiwa akubaliwe dhamana. Mchezo huu wa kuomba hela ili mtu apate dhamana umetamalaki zaidi vituo vya polisi. Wewe kama raia unalotakiwa kujua ni moja tu kuwa hakuna sheria inayomtaka raia kutoa hela ili apate dhamana. Serikalini hakuna risiti ya malipo ya dhamana. Kama wewe utaamua kutoa hela hiyo ujue umetoa kwasababu zako lakini sheria iko hivyo.Ifikie hatua raia wajisimamie kwa kukataa kutoa hela kununua dhamana.

Hakuna kitu ambacho askari anaweza kukufanya ikiwa utakataa kutoa hela kwa ajili ya dhamana. Hakipo kabisa kinachohitajika ni ujasiri wako tu kwa kumwambia askari kwamba sikupi hela kwakuwa dhamana hainunuliwi. Usikubali kutoa hela kwa ajili ya dhamana ndugu ni kosa na hela hizo ni rushwa. Na hiyo ni kwa dhamana zote ya polisi pia ya mahakamani. Katika taratibu za kupata dhamana hamna kulipa hela.

Kusoma zaidi BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad