HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 30, 2015

KITUO CHA JIMOLOJIA TANZANIA KUWEZESHA UONGEZAJI THAMANI MADINI NCHINI

Mkandarasi wa kampuni ya Kiure Engineering iliyofanya Ukarabati Mkubwa katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) cha Jijini Arusha, Oswald Modu ( wa tatu kulia) akimkabithi funguo za vyumba mbalimbali vya kituo hicho, Mkurugenzi wa Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini Amon Makachayo (wa tatu kushoto). Wengine wanaoshuhudia ni baadhi ya watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Wafanyakazi wa kampuni ya Kiure Engineering.
Mratibu wa Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) Mussa Shanyangi (wa pili kulia), akiwaonesha Mkurugenzi wa Manunuzi Wizara ya Nishati na Madini Amon Makachayo (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Habari na Teknolojia Francis Fungameza namna mashine ya kukata mawe inavyofanya kazi.
Baadhi ya Wanafunzi katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) waki polish mawe wakati wa mafunzo. Wanafunzi hao wako katika mafunzo ya ukataji na unga’rishaji madini katika kituo hicho.
Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa   Yahya (kushoto) akimweleza jambo Mkandarasi wa Kampuni ya Kiure Engineering Oswald Modu(wa tatu kulia) wakati wa ukaguzi wa jingo la kituo hicho kabla ya makabidhiano rasmi kufanywa.
Baadhi ya wanafunzi wa kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC) kilichopo Jijini Arusha. Wakiwa katika mafunzo ya kunga’risha madini. Kituo hicho kitawezesha shughuli za Uongezaji Thamani kufanyika chuoni hapo.
Sehemu ya Jengo la kituo cha Jimolojia Tanzania TGC, inavyoonekana pichani baada ya Ukarabati Mkubwa kufanywa na Kampuni ya Kiure Engineering. Jengo hilo limekabidhiwa rasmi kwa kituo hicho mwishoni mwa wiki.
Meneja Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) Idrisa   Yahya (katikati) na ujumbe wa Wizara na Mkandarasi wa Kampuni ya Kiure Engineering wakikagua mfumo wa CCT katika kituo cha Jimolojia Tanzania. (TGC).
Baadhi ya Vinyango vilivyochongwa kwa madini yam awe katika kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad