HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 28, 2015

JAMESON YAKUTANISHA WADAU WAKE

Kampuni ya Pernod Ricard kupitia kinywaji chake cha- Jameson Irish Whiskey iliandaa hafla maalum ya kuonjesha kinywaji chake katika mgahawa wa High Spirit Lounge, jijini Dar es salaam jana.Hafla hiyo iliandaliwa na Balozi wa Jameson Kanda ya Afrika- Nelson Aseka. 

Bwana Aseka, ambaye amepewa mafunzo maalum kutoka kwa wataalam wa kinywaji cha Jameson Irish Whiskey nchini Ireland na mwenye miaka mingi kuwa Balozi wa kinywaji hich alisema, “Jameson inaongoza duniani kwa mauzo katika kitengo cha whiskey kutoka Ireland na imeanza kupata umaarufu nchini Tanzania.

Sababu kuu ya Jameson kuongeza umaarufu wake ni kupitia mbinu zinazotumiwa katika utengenezaji wa kinywaji hiki ambayo inaipa ladha nzuri zaidi. Jameson imezidi kupata ongezeko la mauzo na ubora kwa miaka 24 sasa na inatarajia kuendeleza jambo hili kwa kuingia katika soko la Afrika Mashariki”.

Naye Meneja Ukuzaji Bidhaa wa Pernod Ricard, Bwana Adam Kawa alisema, “ Hii ni moja kati ya hafla nyingi ambazo Pernod Ricard itaandaa katika soko la Tanzania na sio tu kwa kinywaji cha Jameson bali kwa vinywaji vingine kama vile: Ballentine’s, Absolut Vodka, Chivas, Beefeater na Malibu. Na kama mlivyoona katika hafla ya leo tutaendelea kuwafanyia wateja wetu hafla zinazowapatia uzoefu zaidi juu ya bidhaa zetu”.
Balozi Mkuu wa kinywaji cha Jameson Whisk, Nelson Aseka akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuonja kinywa hicho jinsi namna kinavyotengenezwa.Hafla hiyo iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini Dar es Salaam.
Meneja masoko wa Jameson Whisk,Adam Kawa(kulia) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kuonja kinywa hicho iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini Dar es Salaaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika katika hafla ya kuonja Jameson Whisk wakinusa kinywaji cha Jameson Whisk ili kujua harufu yake wakati wa hafla iliyofanyika katika mgahawa wa High Spirit jijini Dar es Salaaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad