Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwaita wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika eneo la Ferry kwa ajili ya safari ya kwenda Bagamoyo na kurudi kwa safari ya majaribio kwa kutumia kivuko cha MV Dar es Salaam alichokikagua leo.
Kivuko cha MV Dar es Salaam kikiwa njiani kuwasili eneo la Magogoni kwa ajili ya kuanza safari ya kwanza ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoani Pwani.Kivuko hiki kinauwezo wa kubeba abiria zaidi ya 300.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakipanda kivuko cha MV Dar es Salaam kwa ajili ya Safari ya majaribio ya kwenda Bagamoyo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akimpokea Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Bagamoyo na Kivuko cha MV Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli katikati akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi kushoto wakiwa safarini kuelekea Bagamoyo Mkoani Pwani, akiwa na Kamanda wa Navy, Meja Jenerali Rogastian Laswai
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliopata fursa ya kupanda kivuko hicho wakitazama madhari ya jiji wakati wakiwa safarini.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amekagua kivuko cha MV
Dar es salaam kinachotarajia kutoa huduma zake kati ya Dar es salaam na
Bagamoyo na kuahidi kuwa kivuko hicho kitaanza kazi siku chache zijazo
mara baada ya kukamilika kwa vituo vya maegesho.
Akizungumza
mara baada ya ukaguzi huo, Waziri Magufuli amewataka wakazi wa Dar es
salaam na Bagamoyo kukitumia kivuko hicho ambacho kitawawezesha kufika
katika maeneo yao kwa haraka na kuepuka usumbufu wa msongamano katikati
ya jiji la Dar es salaam.
“Tumieni
kivuko hiki kwa uangalifu ili kidumu kwa muda mrefu, na sisi Serikali
tutahakikisha tunaweka nauli nafuu ili kuwezesha wananchi wengi kumudu
kutumia usafiri wa kivuko hiki, amesema Waziri Magufuli”.
Waziri
Magufuli amemtaka mkandarasi wa Ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho
ambae ni Kamandi ya Wanamaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ),
kukamilisha ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho mapema iwezekanavyo ili
huduma za usafirishaji zianze mara moja.
Kwa
upande wake Mkuu wa MKoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza
Wizara ya Ujenzi kwa kuwezesha kupatikana kwa kivuko cha MV Dar es
salaam ambacho kitafungua fursa za kiuchumi na kuleta maendeleo kwa
wananchi. Aidha, Eng. Ndikilo ameiomba Wizara ya Ujenzi kuiendeleza
barabara ya Bagamoyo- Zinga hadi Mbegani na kuhakikisha kuwa na usafiri
wa basi moja kutoka Bagamoyo kwenda Mbegani na kuwepo maegesho ya magari
yenye usalama.
Nae
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Eng.
Marceline Magessa, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya kuanza kazi kwa
kivuko hicho yamekamilika ambapo tayari manahodha, mabaharia na mafundi
watakaohudumia kwenye kivuko hicho wameshaajiriwa.
Aidha
Eng. Magessa alibainisha kuwa Kivuko cha MV Dar es salaam
kimetengenezwa na kampuni ya Western Marine Shipyard kutoka Denmark kwa
takriban Shilingi bilioni 8 na kina uwezo wa kubeba abiria 300 wakiwa
wamekaa.
Mkuu
wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ya JWTZ Meja Jenerali Rogasian Laswai,
amemshukuru Waziri kwa kupewa kazi ya kujenga maegesho hayo na kuahidi
kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili wananchi wanufaike na huduma za
kivuko hicho mapema.
Takriban
vituo saba vinatarajiwa kujengwa kwa ajili ya maegesho ya kivuko hicho
ikiwemo Magogoni, K awe, Jangwani, Rungwe Oceanic, Mbweni, Kaole na
Mbegani.
IMETAYARISHWA NA KITENGO
CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI.
No comments:
Post a Comment