HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 19, 2015

WAWILI WAFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA AJALI YA BASI NA LORI ILIYOTOKEA MCHANA WA LEO DODOMA

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

Watu wawili wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya Basi kugongana na Lori ajali iliyotokea tarehe leo tarehe 19/02/2015 majira ya saa saba mchana huko eneo la Vikonje Kata ya Mtumba Barabara ya Dodoma – Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imehusisha Basi lenye namba za usajili T. 663 AXL aina ya SCANIA Kampuni ya KIDIA ONE lililokuwa litokea Dar es Salaam kwenda Mwanza likiendeshwa na ADAM s/o ROBERT, 38yrs, kabila Mnyaturu, mkazi wa Tegeta Dar es Salaam, liligongana uso kwa uso na Lori namba T.469 CFG Scania lenye Tellar T. 756 AZX.

Kamanda MISIME amewataja waliofariki dunia kuwa ni FADHILI S/O HAMIDU SAIDI miaka 36, Kabila Msukuma ambaye ni dereva wa Lori na utingo wa Bus aliyehafamika kwa jina la CHOGO S/O CHIGUNDA, miaka 30, Kabila Muha wote wakazi wa Dar es Salaam.

Majeruhi katika ajali hiyo ni 45 kati yao 34 ni wanaume na 11 ni wanawake; wengine wametibiwa na kuruhusiwa. Waliolazwa ni 24 kati yao wanaume ni 17 na wanawake ni 7.

Kamanda MISIME amesema chanzo cha ajali ni dereva wa Bus Kushindwa kuchukua tahadhali wakati wa kulipita gari lingine “over take”, na kusababisha ajali hiyo.

Aidha Kamanda  MISIME ametoa wito kwa madereva kuwa na udereva wenye tahadhali na kuzingatia sheria za usalama barabarani, kwani dereva huyu wa basi angezingatia hilo ajali hii haingetokea na hatakama ingetokea madhara yake hayangekua makubwa kiasi hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad