HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 27, 2015

RITA wazindua mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Wilaya ya Kinondoni

Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni,Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mkakati huo,akishirikiana na Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yussuf Mwenda,Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Phillip Saliboko pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mhandisi Mussa Natty. Uzinduzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni jijini Dar es salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Phillip Saliboko akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo,uliofanyika leo Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni.
Mgeni Rasmi katika Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni,Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni jijini Dar es salaam.Wengine pichani toka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddi Azzan,Meya wa Manispaa ya Kinondoni,Mh. Yussuf Mwenda pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),Phillip Saliboko.
Sehemu ya Wajumbe wa Elimu kutoka katika Kata mbali mbali za Wilaya ya Kinondoni,wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi kwenye Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya hiyo.
Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro akikabidhi vyeti vya kuzaliwa kwa baadhi ya wanafunzi kutoka Shule za msingi za Wilaya ya Kinondoni,wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni.
Meza kuu ikipata picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi hao pamoja na walimu wao.
 Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Dkt. Asha-Rose Migiro (katikati) akimsikiliza Msajili wa Vizazi na Vifo (RITA) Manispaa ya Kinondoni,Mariam Ling'ande (kushoto) wakati akielezea juu ya namna RITA inavyotunza kumbukumbu,wakati wa Uzinduzi wa Mkakati wa Usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.Uzinduzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Turiani,Magomeni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad