HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 20, 2015

MH. LOWASSA ASHIRIKI KWENYE MAZISHI YA MWAKILISHI WA JIMBO LA MAGOMENI ZANZIBAR LEO

Waziri mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka udogo kaburini wakati wa mazishi ya Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanzibar ambaye pia alikuwa Mnadhimu na Katibu wa Wakilishi wa Chama Cha Mapinduzi katika Baraza la wawakilishi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mh. Salmin Awadh Salmin kijijini kwao Makunduchi leo Ijumaa.Marehemu Salmin Awadh Salmin alifariki ghafla jana wakati akiwa kwenye kikao katika Afisi kuu ya CCM kisiwandui,mjini Unguja Zanzibar.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Waziri mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa mara baada ya mazishi ya Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Zanziba, Mh. Salmin Awadh Salmin kijijini kwao Makunduchi leo.
 Waziri mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad