HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 20, 2015

KWA ULISOKISEMA NDUGU HENRY MDIMU,NANYANYUA MKONO JUU KUUNGANA NAWE

"Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua.
Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza.

Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA.

Wanaoniunga mkono mikono juu" Mwisho wa kunukuu.

Nikiwa kama Blogger na Mwanahabari Mwenza wa rafiki yangu na Kaka yangu Kipenzi,Henry Mdimu aliejitolea kuwa Balozi,nanyoosha mkono juu kwa kuunga mkono kupiga vita vikali mauaji ya ndugu zetu wenye Albinism.kwani wao pia ni Binadamu kama tulivyo mimi na wewe.JAMANI SASA BASI,NA KILA MMOJA WETU AWE MLINZI KWA NDUGU ZETU HAO.
 Mimi na Henry Mdimu ni dugu moja.
 Mie,Mdimu na Swahiba Cathbert Kajuna,sie wote ni wanablog na tunapendana sana tunafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.
Misele na Kaka Mdimu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad