HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 21, 2015

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYO HUKU USWAZZ KWETU

 Huku Uswazz kwetu mambo ni mukide kweli kweli,tukianzia mtaa huu wa kwa kina Rama Boy ambao una kimtaro kifupi kinachoanzia kwenye nyumba ya Mama nanihii na kuishia hapo.lakini majirani wote huendelea kumwaga maji katika kimtaro hicho na ilihali kinaonekana kabisa kutuama.
 Dada pale keshafanya yake tayari kwenye kimtaro hicho.
 Hivi ndivyo mambo yalivyo hapo.
 Mihogo ya kukaanga ni menyu yetu huku uswazz hasa kwa kunywea chai asubuhi.
 Paka wa mzee nanihii kwa mbwembwe tu hajambo,eti nae hapo ndio anaangalia maji kama vile sie tuendavyo bichi.
 Njia zetu huku Uswazz.
 Hawa Bata leo wamepatikana,maana wanapenda kama nini kushinda kwenye maji machafu.
 Safari ya Dampo kutupa taka.
 Mitaro ya kujitolea ipo ya kutosha tu huku Uswazz kwetu.
 Mandhali ya Maliwato.
 Kikwangua anga kinachomoza uswazz kwetu.
 Mdau akienda zake kwenye misele.

 Ukiona hivi tu jua mambo yalishaharibika usiku wa leo.

 Swimingi pulu ya hatari nje.

2 comments:

  1. Haya. Ndio maisha bora kwa kila Mtanzania? Sasa hapo magonjwa ya milipuko. Kama kuhara.kupindupindu. Maralia. Homa ya Dengue.

    ReplyDelete
  2. Ninachowapendea Mimi watanzania si watu wa kuhoji Na kudai haki Zao za msingi,kuanzia serikali za mtaa mpaka serikali kuu.watanzania wapo mfano wa karai la kujengea,hua lina umuhimu Tu pale nyumba inapojengwa ,ikishakamilika hutupwa ktk ghala.asilimia 75 ya watanzania wanaishi ktk mazingira yasiyo rasmi ,yasiyo huru Na salama kwa kukosa miundo mbinu.watanzania wengi hawana desturi ya kujifunza haki Zao zinapatikana wapi Na kwa njia ipi.chaguzi za serikali kuanzia mtaa mpaka serikali kuu tangu uhuru mpaka sasa hazijafikia kiwango stahiki kwa mujibu wa nchi Na malighafi zake zilivyo Na hilo watanzania hawajachukua hatua inayofaa mpaka kesho.jamani Mimi Ni mtanzania niliezaliwa tandale bondeni miaka 39 ilyopita Na kusoma shule ya msingi turiani (sijui sasa km yaitwa hivyohvyo) ilyo kata ya ndugumbi magomeni.nilizaliwa ktk familia duni Sana ya watoto 9 na nikasoma ktk mazingira duni Sana na kufeli darasa la saba(siamini km nilifeli ila naamini nilifelishwa) nilipomaliza shule sikuweza endelea na masomo.mpaka mwaka 1982 ndipo nilipofanikiwa kuoa binti wa kifaransa niliyekutana nae arusha na kuweza kuondoka nchini.kwa maana hiyo nayajua maisha yetu.sasa Ni mtu mzima nilie miliki PhD ktk udaktari . Ndugu zangu tuamke ,tuihoji serikali ,tuwahoji viongozi watekeleze ahadi Zao.hali inatisha kuona kiwango cha umaskini kinakua leo hata kesho .imekua sasa alienacho anazidi kuwa nacho na asienacho anazidi kuzama.kila raia anapenda maisha Safi.ile kuitwa uswazi Ni ukosefu Tu wa kipato.nawaamsha ndugu zangu.Asanteni.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad