HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 18, 2015

DAWASCO KULA SAHANI MOJA NA WEZI WA MIFUNIKO YA CHEMBA ZA MAJI

Licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa kuzuia uhujumu miundombinu ya Majisafi na wizi wa Maji, hujuma nyingine kubwa ya chuma chakavu za MAJITAKA imebainika baada ya DAWASCO kukamata mifuniko ya Majitaka katika kiwanda cha nondo cha IRON&STEEL cha jijini Dar es salaam.

 Vyuma Chakavu hivyo ambavyo ni mifuniko ya chemba za Majitaka za DAWASCO zimebainika baada ya uchunguzi wa kina na taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu upatikanaji wa mifuniko hiyo kiwandani hapo.

Afisa Uhusiano wa DAWASCO Bi Everlasting Lyaro alisema ilibidi watumie mbinu mbadala ili kubaini biashara hiyo iliyokuwa ikiendelea kiwandani hapo, ambapo kwa kushirikiana na Polisi kutoka kituo cha kijitonyama na Afisa Mtendaji wa kata ya Mikocheni waliweza kuvamia kiwanda hicho na kukuta mifuniko mingi ya chemba za Majitaka ambazo ni mali ya DAWASCO.

“Bei ya mfuniko mmoja wa Majitaka huwa tunanunua kati ya Tsh laki tano hadi sita (500,000 -600,000) kutegemeana na ukubwa wa mfuniko, lakini hawa wakishaiba huwa wanaenda kuuza sh 500 kwa kilo hivyo unakuta gharama kubwa inabaki kwetu sisi tunaotoa huduma hii” alisema Lyaro
“mifuniko ya chemba za Majitaka ni muhimu kwa uhifadhi wa Majitaka na pia kuzuia uchafu huo kutapakaa ovyo mitaani, hivyo kuendelea kushamiri kwa biashara hiyo kunatupa wasiwasi wa uwezekano wa magonjwa ya mlipuko utakaosababishwa na utiririshwaji wa Majitaka ovyo mitaani” alifafanua Lyaro Aliongeza kwa kusema mapambano ya uhujumu katika miundombinu ya DAWASCO bado ni kubwa na inahitaji ushirikiano wa pamoja kati ya wananchi, viongozi husika pamoja na DAWASCO katika kulinda na kuhifadhi miundombinu ya Majisafi na Majitaka.

Katika tukio hilo Meneja Mkuu wa kiwanda hicho Raju N. Chita na Meneja utumishi Idrisa Ally wamekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kijitonyama na kufunguliwa Jalada namba KJN/1786/2015 kwa hatua zaidi kisheria.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad