HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 5, 2015

ASKARI POLISI ALIYEUAWA KIKATILI AAGWA LEO MKONI DODOMA

Kamanda wa Polisi nchini,IGP Ernest Mangu akiongoza waombelezaji wengine kuaga mwili wa Askari Polisi mwenye namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI Mkoani Dodoma.
OCD - Thadeus Malingumu (SP) akisoma wasifu wa marehemu PC Joseph.
Wachungaji wa kanisa la KKKT wakiombea mwili wa marehemu.

Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kama Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema kama alivyotoa taarifa jana tarehe 04/02/2015 kuhusiana na kuawa kwa Askari wetu Namba G. 7168 PC JOSEPH ISACK SWAI huko Chango’ombe ya juu Mkoani Dodoma na mtu aliyefamika kwa jina la TISSI S/O SIRIL MALYA; Jeshi la Polisi Mkoa wa Dododoma lilianza msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo baada ya kufanya kitendo hicho cha kinyama cha kumkata kata kwa panga kichwani na mikononi Askari huyo.

Kamanda MISIME amesema majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili Mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua Askari.

Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki.

Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua.

Ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi. Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad