Mtoto wa miaka mitano aliefahamika kwa jina la Alex Nash mwenye umri wa miaka mitano (5),ametakiwa kulipa faini ya paundi takribani 16 kwa kushindwa kuhudhuria mwaliko alioukubali wa hafla ya kuzaliwa kwa rafiki yake.
Aidha wazazi wa mtoto huyo wametishiwa kufunguliwa mashtaka kama hawatalipa faini hiyo iliyotokana na mtoto wao kutohudhulia hafla hiyo.
Mtoto Alex Nash anaetokea Cornwall, alialikwa katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya krismasi ya mwaka uliopita na aliukubali kwamba angehudhulia hafla hiyo,lakini siku ya tukio hakutokea.
Faini hiyo ya £15.95 ilitumwa na mama wa rafiki yake huyo aitwae Julie Lawrence, ambaye alisema kutohudhuria kwa Alex kumemtia hasara na kwamba wazazi wake walikuwa na wajibu wa kumwambia kwamba kijana wao hatafika katika hafla hiyo.
Baba yake Alex, amesema kwamba watafikishwa katika mahakama ya madai madogo kama hawatalipa faini hiyo.
Wazazi wa Alex waliupokea mwaliko huo na walikubali mtoto wao kuhudhuria hafla hiyo iliyokuwa inafanyika Plymouth, Devon kabla ya krsimasi.
Lakini kutokana na mambo ya hapa na pale,waligundua baadae kwamba mtoto wao alitakiwa katika eneo jingine ambako ni kwa babu yake na ndiko alikoelekea.



No comments:
Post a Comment