Kamera yetu leo imebahatika kukatiza maeneo haya ya Tandale Soko la Mitumba,kama unaelekea Manzese Uwanja wa Fisi.hili ni moja ya masoko ya kitambo hapa jijini Dar na linasifika kwa kuwa na mitumba mikali mikali.

Soko hili linabiashara kede kede na nyingi ni mitumba ya vitu mbali mbali kama vile Nguo,Viatu,Mabegi,Mashuka na vitu vingine vingi.

Hata kama wewe ni mfuasi wa nanihii,basi zile yunifomu huwezi kukosa maana pia zipo kibao.

Kwa wanaotaka kuolewa hivi karibuni,mashera ndio kama hayo tena na mengine yanagombaniwa.wahi bahati yako.
Hapa mzigo wa zile za kina mama umeshuka muda si mrefu.
Baba akimchagulia mama zile nanihii.
Hapa ni mwendo wa sagula sagula..haya yote yanapatikana Tandale jamani.
No comments:
Post a Comment