![]() |
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza maneno ya Utangulizi kabla ya kukabidhiwa vifaa vya kukabiliana na ujangili kutoka na serikali za Marekani na Ujerumani katika hafla hiyo. Kulia ni Balozi wa Mrekani Mark Childress na waili kulia ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke
|

Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress akizungumza kabla ya kutiliana saini na Nyalandu mkataba ya kukabidhiana vifaa hivyo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke

Balozi wa Marekani Mark Childress na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu wakitiliana saini mkataba wa Marekani kuipa Tanzania msaada wa mafunzo yakiwemo ya kikomandoo kwa askari wa wanyamapori na vifaa vya kisasa vya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous leo.

Waziri Nyalandu akibadilishana hati na Balozi wa Marekani, Mark Childress baada ya kusaini mkataba huo. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani Egon Kochanke

Waziri Nyalandu akibalidilishana hati na Balozi wa Ujerumani Tanzania Egon Kochanke, baada ya kutiliana saini mkataba wa ujerumani kuipa Tanzania msaada wa vifaa vya kisasa vya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyama ya Selous leo

Vifaa mbalimbali vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na majangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous

Askari wa Wanyamapori Anita Albert akijaribu kionambali ambacho ni miongoni vya vifaa vilivyotolewa kwa Tanzania na Seriali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili

Askari wa wanyamapori wakikagua mahema ambayo ni miongoni mwa vifaa vya kisasa vilivyotolewa na serikali za Marekani na Ujerumani kwa ajili ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya wanyamapori ya Selous.

Meneja
wa Mbuga ya wanyama ya Selous, Benson Kibonde akimpatia maelezo kuhusu
masalia ya injini ya mvuke iliyoachwa na Wajerumani, kwa Waziri wa
Maliasili na Utalii Lazao Nyalandu (kushoto), waziri huyo alipofika
katika mbuga hiyo, kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kupokeavifaa vya
kukabiliana na ujangili vilivyotolewa na serikali za Marekani na
Ujerumani kwa ajili ya Mbuga ya Selous leo


Waziri
Nyalandu akitembela maeneo mbalimbali ya mbuga hiyo ya Selous kabla ya
kukabidhiwa vifaa hivyo ya kukabiliana na ujangili katika mbuga ya
wanyama ya Selous leo. anayemuongoza na Meneja wa mbuga hiyo

![]() |
Mkurugenzi
wa theNkoromo Blog, Bashir Nkoromo, ambaye alialikwa kwenye hafla hiyo,
akitazama mto Ruaha unaopita katika mbuga ya Selous
|

Waandishi wa habari wakiwa kwenye hafla hiyo
Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog
No comments:
Post a Comment