HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 20, 2015

KILICHOTOKEA MCHANA WA LEO MAENEO YA CHANG'OMBE JIJINI DAR

 Kama ilivyo kawaida ya watu wa maeneo mengi hapa nchini,kwamba likitokea la kutoka basi huwa ni faida kwa watu wengine.Mchana wa leo katika Makutano ya barabara ya Nyerere rodi na Kawawa rodi,gari ndogo aina ya Toyota Hilux iliyokuwa imebeba Vioo ilipatwa na mkasa na kupelekea mzigo wa vioo hivyo kuanguka katikati ya barabara na kupasuka,hali iliyowapelekea vijana wanaofanya biashara za mikononi (maarufu wa machinga) katika eneo hilo kuingia barabarani na kuanza kujibebea mabaki ya vioo hivyo kama ionekanavyo pichani hapa.hali iliyopelekea kwa magari mengine yalikuwa yakiitumia njia hiyo kuwakwepa vijana hao ili waendelee na kazi yao ya kujisevia. 
 Hali hiyo ilidumu kwa muda kidogo,hali iliyopekea Askari wa usalama barabarani kuyaongoza magari kupita pembezoni mwa barabara hiyo ili kuwaacha vijana hao ambao hawakutana kusikia la muadhini wala la mnadi swala.
 Kwa hiki kinachoonekana hapa ni kama vile waliombea litokee hilo.
 Vijana hao wakiendelea kujibebea vioo vyao hivyo,huku mzee wa Feva akiendelea kiwapiga chabo.
 Kazi ikiendelea.
Walioridhika waliondoka na waliokuwa bado hawajapata wanachokitaka waliendele.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad