HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 27, 2015

BALOZI WA JAMHURI YA KOREA AMTEMBELEA WAZIRI WA UJENZI OFISINI KWAKE JIJINI DAR

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akizungumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea, Chung Il kuhusiana na mambo mbalimbali kuhusu sekta ya Ujenzi pamoja na mchakato wa Ujenzi wa Daraja jipya litakalopita baharini pembezoni mwa daraja la Selander.Daraja hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7.2 na uwezo wa kupitisha magari zaidi ya 61,000 kwa siku. Ujenzi wa Daraja hilo utaanza muda wowote kuanzia sasa. Daraja hilo litakuwa na njia nne za magari pamoja service road njia za waenda kwa miguu kila upande.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiagana na Balozi wa Jamhuri ya Korea Chung Il mara baada ya kufanya mazungumzo ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi huyo wa Jamhuri ya Korea Chung Il pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Musa Iyombe na Mkurugenzi wa Barabara Eng. Ven Ndyamukama. Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini- Wizara ya Ujenzi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad