HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 26, 2015

ALIYEVUNJIKA TAYA APATA MSAADA WA KIFEDHA AOMBA NDUGU ZAKE WAJITOKEZE

Gabriel Ng'osha akimkabidhi Bi. Masumbuko ambaye ni msimamizi wa wodi ya Sewa Haji namba 23 kwenye  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili pesa taslimu masaada wa laki moja na elfu kumi na nane (118,000) leo kwenye hospitali hiyo.
Emmanuel Nelson akiwa amelala kwenye wodi Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Emmanuel Nelson mwenye umri wa miaka kati ya (30 - 35), ambaye ni  mzaliwa wa Mbamba Bay, Ruvuma na ambaye wazazi wake wanaishi Dodoma, aliyekuwa anaomba msaada wa kutibiwa taya ambalo limevunjika. Leo amepatiwa masaada wa laki moja na elfu kumi na nane (118,000) kwa ajili ya matibabu kutoka kwa wasamalia wema kupitia blog yetu ikishirikiana na global publisher.
Nelson ambaye alishindwa kuongea akiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alifikishwa na   polisi wa kituo kidogo cha Pangani, Ilala, jijini Dar es Salaam, Januari 15 mwaka huu baada ya kuokotwa barabarani, inasemekana alivunjwa taya hilo kwa kupigwa na watu wasiojulikana.
Pia Emmanuel Nelson amesema kuwa anawaomba ndugu zake popote walipo wajitokeze ili waweze kumsaidia maana hali yake sio nzuri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad