HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 5, 2014

TFF YATANGAZA RASMI RATIBA YA MASHINDANO YA KOMBE LA WANAWAKE TAIFA

 Rais Wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mh Jamal Malinzi akizungumza na wanahabari leo katika ofisi za TFF kuhusu kampuni ya Proin Promotions ltd kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa, mashindano hayo yanatarajiwa kuanza tarehe 28 Disemba kwa kushirikisha timu kutoka Mikoa yote ya Tanzania. Mashindano hayo yatazinduliwa Mkoani Mwanza kwa kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara. Kushoto kwa rais wa TFF ni Rose Kissiwa ambae ni mwakilishi wa Chama cha Mpira wa wanawake Tanzania.Na Kulia ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza ambao ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Wanawake Tanzania
 Rais wa TFF akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na Kombe la Wanawake Taifa ambapo ni mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
 Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza akizungumzia jinsi kampuni ya Proin Promotions Ltd ilivyoona umuhimu wa kuchangia katika kuinua soka la wanawake nchini na kuamua kudhamini Shindano hilo lijulikanalo kama Kombe la Wanawake Taifa ambalo litaanza rasmi tarehe 28 kwa mechi ya uzinduzi kati ya Mwanza na Mara huko Mkoani Mwanza
Bi Rose Kissiwa, Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania akizungumzia juu ya udhamini uliotolewa na kampuni ya Proin Promotions Ltd katika kufanikisha Mashindano ya Mpira wa miguu kwa Wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo uzinduzi wa Mashindano hayo yatafanyika Jijini Mwanza kwa kuzikutanisha TImu za Mwanza na Mara.Picha zote na Josephat Lukaza  wa http://www.josephatlukaza.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad