Kampuni Tan Communication Media inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina "Kampeni ya USHINDI"linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho Robert Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione kutengwa
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na tukifanya hivi watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio 5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful company,World garden.(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Wadau wakiwa wanafatilia shindano
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment