Mama wa kijana anayeugua ugonjwa wa kifafa amekataa kumpa mwanawe wa kiume bangi kama matibabu kupitia moshi na mvuke wake. Mtoto huyo anapaswa kutumia Bangi kama dawa kupambana na ugonjwa wake huo kwa maagizo ya daktari.
Liam McKnight mwenye umri wa miaka sita anapenda kucheza na ndiye wa kwanza kila mara kukimbia kuelekea mlangoni pindi asikiapo kuna mgeni anagonga mlango.Mama mzazi wa Mtoto huyo aliefahamika kwa jina la Mandy, anasema kuwa mwanawe anapenda kujua nani anawatembelea.
Familia hiyo ya McKnight inayoishi jijini Otawa nchini Canada ina wageni wengi wanaowatembelea,wengi wakini ni wakutoka kwa wanachama wa kukindi cha dansi anachoshiriki binti yake ambaye ni Dada wa kijana Liam,na hata wauguzi wa kutamka,wa kunyosha viungo vya mwili,wataalam wa kusikiza-wote wanaomtembelea Liam.

Liam ana ugonjwa unaojulikana kama Dravet ambao ni aina kali sana ya kifafa.Afya yake hudhoofika mara kwa mara lakini baada ya kufanyiwa majaribio kadha wa kadha ya matibabu ya ugonjwa huo, angalau hali yake imeimarika kidogo.
Mamake Liam humpa mafuta ya Bangi, ambayo yametolewa kwa sehemu changa sana ya mmea huo.
Mwezi Juni mwaka huu,siku kabla Liam kuanza kutumia mafuta hayo ya Bangi,(iliyotengezwa kutoka kwa aina ya bangi yenye ufanisi) alizirai kama mara 67. Katika siku kumi zilizofuatia alizirai tu mara moja.
Tatizo ni kuwa matibabu ya Liam ni haramu. Kutumia dawa inayotengezwa kwa Bangi inakubalika Canada lakini lazima iwe tu majani ya Bnagi yaliyokaushwa au mvuke wa majani hayo.
Kwa Mandy hilo haliwezakani kwa mwanawe kuvuta moshi wa Bangi akiwa umri huo mdogo.
Mtoto mdogo anawezaje kuvuta Bangi? anauliza Mama Liam.
Mapema mwaka 2001, Canada iliruhusu wagonjwa wanaohisi uchungu mwingi kutumia Bangi kama matibabu. Lakini hakuna majaribio yaliyofanyiwa mafuta ya Bangi kujua usalama wake kwa afya ya mtu.
Liam ana umri mdogo sana lakini anaweza kutumia mvuke wa Bangi lakini mama yake Liam anasema vipimo vinavyofaa kwa afya ya Liam ni vya mafuta ya Bangi.
Mamake Liam aliwahi kuiandikia serikali Barua kuielezea kuhusu masaibu yake kuhusiana na matibabu ya Liam. Lakini waziri wa afya alimjibu kwa kusema anaelewa masaibu ya mtoto Liam wakati akikabiliana na ugonjwa wake hatari wa kifafa. Lakini alisisitiza kuwa hadi leo serikali bado haijaidhinisha matumizi ya mafuta ya Bangi wala uuzaji wa mafuta hayo nchini Canada.
Matumizi ya mafuta ya Bangi, yaliruhusiwa mjini Minnesota Marekani mwezi Mei, lakini sheria hiyo haitaanza kutumika hadi Julai mwaka 2015.
Sheria za Bangi kote duniani zinatofautiana.
Mama yake Liam anafahamu kuwa anavunja sheria pamoja na kufahamu athari za kutumia mafuta ya Bangi. ''Je nahofia kuwa navunja sheria? ndio. Lakini nahofia zaidi ikiwa hatutafanya chochote hali ya afya ya mtoto wangu itazorota.
Kwetu Mafuta ya Bangi ndio tiba anayohitaji mwanangu. Hatukuwa na mda wa kusubiri majaribio kufanywa. Kwa kila siku, Liam hula kijiko kimoja cha Bangi ikiwa imechanganywa na mafuta ya nazi.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment