Katika pita pita zetu za Mtaa kwa Mtaa,tuliibuka maeneo ya Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam na kukutana na mziki huu mnene na wakutatanisha uliozikutanisha gari mbili,ukiangaliwa kwa makini utabaini kuwa hili gari kubwa lenye nambari za Usajili T 544 CKG mali ya Kampuni ya Azania lilikuwa lipo kwenye njia yake halali kabisa kuelekea Buguruni na huyo mwenye Gari ndogo lenye nambari za Usajili T806 AVT anaonekana akielekea Ubungo lakini katika njia ambayo aimrusu yeye kupita.Kilichotokea hapo ndio kama inavyoonekana pichani.Sasa sijui huyo mwenye hiyo gari ndogo alijiona anaendesha Boda boda....!!! Maana hapo alipotaka kupita hata hapaelezeki.
Hapa hata sijui walitaka kupishana vipi??
Mashuhuda wa tukio hilo wakiendea kushangaa wanachokiona,maana hata haieleweki huyo Dereva alikuwa anawaza nini??
Hebu ona.
Mzee wa Feva akifanya yake kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Makubwa ametumia right hand driving
ReplyDelete