HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 1, 2014

IBADA YA SHUKRANI za dhati kwenda kwa wadau mbalimbali

kansolele
Inaniwia vingumu sana kutoa shukrani kwa mtu mmoja mmoja au makundi kutokana na ushirikiano wenu katika kipindi kigumu cha msiba na mazishi ya mpendwa mume wangu na mwenyekiti wa Dorka catering na Dorka group of company Marehemu Dr kephas kansolele Ntevi kwaniaba ya familia yangu .

Ninapenda kutoa shukrani za dhati kwa wote walio shiriki kwa njia moja au nyingine kwa kipindi chote cha msiba wa mume wangu.Kiukweli tulipatwa na kigugumizi ambacho hakisemeki Ingawa nyote mnastahili kushukuriwa lakini ningependa kutoa shukrani zangu za peke kushukuru madaktari wa Muhimbili na manesi kwenye kitengo cha I.C.U , Dr Kalianyama mlifanya kazi usiku na mchana kuokoa maisha ya mume wangu lakini mungu alimpenda zaidi, kanisa la Good News Mission Tanzania Pastor kiongozi Jeong na ma pastor na waumini wote hamkuchoka kutuombea na bado mnatuombea tuna shukuru sana, Service Provider wezangu kiukweli mmenionyesha upendo ambao hausemeki, Marafiki zangu na wa familia mlikua na sisi usiku na mchana hamkutuacha, Networks wote waliokua wana shirikiana na mume wangu .

Blogs mbalimbali, majirani zetu wa mwenge na Bahari beach , Familia ya Ntevi, Familia ya Wakaombwe na ya Mzee Massau tunapenda kuwashkuru wote kwa upendo na faraja zenu, Sina maneno mazuri ya kuonyesha shukurani zetu za dhati kwa niaba yangu na wanangu, tunaomba mpokee shukurani zetu mwenyezi mungu awaongezee pale mlipo toa. 

Tutakua na Ibada ya shukurani nyumbani kwa marehemu kunduchi njia panda ya madini.
Ratiba itakua kama ifuatavyo
Tarehe ::5/12/2014 mkesha Ibada na dinner (BBQ Night)
Tarehe ::6/12/2014 kuanzia saa 2 asubuhi wageni kuwasili na saa nne (BRUNCH) Hadi saa tano mchungani wa Good News mission atapowasili na saa tano na nusu ibada neno la shukrani ya familia
kwa mawasiliano ::+255718 661 705 / +255717 056 598
Bwana ametoa na ametwaa
Wote mnakaribishwa kushirikiana na sisi kumtolea mungu shukrani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad