Baada ya kukosekana mvua kwa muda mrefu katika maeneo yanayozunguka Mlima Kilimanjaro kutokana na uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na ukataji wa miti hovyo,sasa hali ya zamani imeanza kurejea.
Wananchi ambao awali walilazimika kuingia
ndani ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ajili ya ukataji
wa majani kwa ajili ya mifugo yao ,sasa hivi hali ni tofauti wamekuwa
wakikata majani waliyootesha wenyewe na kustawi kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha katika maene hayo,na sasa hawaingii tena
katika hifadhi ya taifa ya mlima Kilimanjaro kukata
majani.
Mmoja wa wafugaji Ludovick Meela Serik akifurahia hali ya upatikanaji wa majani kwa ajili ya mifugo yake ilivyo sasa.
Majani kwa ajili ya mifugo kwa sasa yanapatikana na hata afya sasa imeanza kurejea tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Kina mama ambao wamekuwa wakijishughulisha
na kilimo cha Mboga mboga wamekuwa wakifanya biashara vizuri kutokana
na upatikanaji wa mboga ambazo kwa sasa zimekuwa zikipatikana kwa
wingi tofauti na hapo awali ambapo wamekuwa wakisafirisha mboga hizo
hadi nchi jirani ya Kenya.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali
la FLORESTA ,Richard Mhina akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)
namna ambavyo shirika lake lilivyo saidia vikundi mbalimbali katika
kampeni za utunzaji Mazngira kwa kuotesha miti pamoja na uanzishwaji
wa vitalu vya miti.Picha na Dixon Busagaga wa
kanda ya kaskazini.
No comments:
Post a Comment