HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 21, 2014

KAMERA YA MTAA KWA MTAA NA TASWIRA ZA ENEO LA MWANJELWA MSIMU HUU WA SIKUKUU.

Libeneke la Mtaa kwa Mtaa Blog likiwa katika matembezi yake ya kusaka chochote ili lisilale njaa,leo limezama moja kwa moja ndani ya maeneo ya Mwanjelwa jijini Mbeya na kuzinasa taswira mbalimbali za wafanya biashara ndogo ndogo jijini humo wakijitafutia chochote kitu ili mkono uende kinywani msimu huu wa sikukuu za xmasi na mwaka mpya katikati ya barabara inayo unganisha maeneo ya Mwanjelwa na Makunguru.
 mjomba ndani ya mpama akijaribu kuweka sawa biashara yake.
          vijana wakipagawisha wateja wao juu ya gari eneo hilo.
 pisha nikupishe ndio inayofanyika hivi sasa katika eneo hili katika kusalula pamba za sikukuu.
 dogo mgongoni akimnong'oneza mazaake juu ya kikali alicho kiona na kusemaa "mama mii aonaa iyee atuu nzhuliii mamaa"
             pilika  zikiwa zime pamba moto eneo hilo la mwanjelwa.
         wakina mama hawa nao wakiwa wamefungua belo la mitumba nje ya nyumba yao kandokando ya barabara huku,huku wakibadilishana mawazo mbalimbali juu ya sikukuu itakuwaje kwa upande wao wachange au wasichange.
Kameramani wa libeneke hili la Mtaa kwa Mtaa chini Kampuni ya Michuzi Media Group Kanda ya nyanda za juu Kusini, Fadhiri Atick a.k.a Mr Pengo akiwa katika harakati za kujua bei ya buti kwa ajili ya maandalizi ya sikukuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad