Bia ya Castle Lite, inazozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
leo imefunga rasmi promosheni ya "Lite Up The Weekend" ambayo imeendeshwa
kwa muda wa miezi mitatu katika mikoa nne ya Tanzania ambayo ni; Mbeya, Mwanza,
Arusha, Dar es Salaam.
Washindi walioshiriki katika promosheni hii, ambayo ilikua
ikitangazwa kupitia vipindi mbalimbali katika vyombo vya habari nchini, walipata fursa
ya kujishindia zawadi kemkem, ambayo vilevile washindi 60 walijishindia pesa taslimu
TZS. 100,000. Wote walioshiriki promoshini hii waliingizwa kwenye droo kubwa
kuwania nafasi ya kujishindia tiketi ya ‘VIP ya Castle Lite Yacht Party.’
Akizungumuza na waandishi wa habari, Meneja wa bia hiyo ya Castle Lite, Bw. Geoffrey
Makau alisema; ‘tunavyo fikia tamati, napenda kuwapongeza washindi wa droo kubwa
ambayo ndiyo droo kubwa ya mwisho ya kampeni hii, ambayo ilifanyika wiki hii kubaini
washindi wa zawadi kubwa. Wao na wenzi wao moja, watasherehekea wikendi nzuri
kupitia bia ya Castle Lite. Gharama zote, ikiwepo usafari, hoteli, chakula cha jioni,
burudani katika bar yakifahari jijini Dar es Salaam, zote zitalipiwa na bia ya Castle Lite.
Zaidi ya hapo, hiyo furaha yote itaongezeka pale ambapo washindi watazungushwa
kwenye boti yakifahari wakiangalia mandhari nzuri ya usiku ya jiji la Dar es Salaam.
Ndani ya boti hilo kutakua na muziki, na chakula. Mwisho wa yote boti itasimama
iwashushe washindi hao kwenye sherehe yakumalizia wikendi ya VIP na Castle Lite.
Meneja wa Castle Lite, anawashukuru wote walioshiriki kwenye promoshini ya Castle
Lite, “Lite Up The Weekend’ nakutoa mwito kwa wapenzi wa Castle Lite waendelee
ku ‘Lite Up The Weekend’ na bia ya Castle Lite.
Meneja msaidizi wa Castle lite,Victoria Kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya kupatikana kwa washindi wa shindano la bia ya castle lite Yatch party ambapo jumla ya washindi kumi na tano nchi nzima wamepatikana .Pembeni yake ni meneja wa bia ya Castle lite Geofray makau.
Meneja wa Castle lite Geofray Makau akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam juu ya kupatikana kwa washindi wa shindano la bia ya castle lite Yatch party ambapo jumla ya washindi kumi na tano nchi nzima wamepatikana .Pembeni yake meneja msaidizi Victoria Kimaro
No comments:
Post a Comment