Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation),Bi. Brigitte Alfred akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo.Taasisi ya BAF kupitia Mpango
wake wa JA (Juniour Achievement) imeweza kuelimisha vijana 50 wenye
ulemavu wa ngozi katika mpango wa kutoa elimu ya kujitambua,
ujasiriamali na stadi za biashara ili waweze kuthubutu, kuanzisha na
kuendeleza biashara na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazo wapa
ajira, kipato na kuinua ustawi wa maisha yao na familia zao.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation),Bi. Brigitte
Alfred akimtumza mmoja wa vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao
wako chini ya Taasisi hiyo,aliekuwa akighani shairi alilolitunga,wakati
wa hafla ya kusherehekea Mafanikio ya Vijana hao iliyofanyika leo kwenye
Viwanja Makumbusho,Jijini Dar es Salaam.
Kijana mwenye ulemavu wa ngozi (albino) akighani mashairi yake.
Mwenyekiti
Mtendaji wa Taasisi ya Brigitte Alfred Foundation,Bi. Brigitte Alfred
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Pugu waliofika kwenye hafla hiyo ya kusherehekea Mafanikio
ya Vijana,yaliyofanyika leo kwenye Viwanja Makumbusho,Jijini Dar es
Salaam.
Mie na Wadau wengine tuliofika kwenye hafla hiyo,tukiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti Mtendaji wa Taasisi ya BAF (Brigitte Alfred Foundation) na Miss Tanzania 2012,Bi. Brigitte Alfred pamoja na baadhi ya vijana wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao wako chini ya Taasisi hiyo.






No comments:
Post a Comment