HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 19, 2014

Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Zantel zakabidhiana mkataba ya maelewano ya kibiashara

 Mkurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme (kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiana mkataba wa maelewano ya kibiashara kati ya Taasisi zao. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Mambo ya Ufundi wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Moncef Mettiji.
Mkurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme (kulia) na Ofisa Mkuu wa Mambo ya Ufundi wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Moncef Mettiji (kushoto), akimwakilisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, wakibadilishana mkataba wa maelewano katika ushirikiano wa kibiashara kwa mambo ya mawasiliano, ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Mkuu, Uhusiano na Serikali wa Zanztel, Charles Jutta.
Mkurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme (kulia) na Ofisa Mkuu wa Mambo ya Ufundi wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Moncef Mettiji (kushoto), mwakilisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, wakiupitia mkataba wa maelewano katika ushirikiano wa kibiashara kwa mambo ya mawasiliano, mara baada ya kukabidhiana, katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja Mkuu, Uhusiano na Serikali wa Zanztel, Charles Jutta.
Ofisa Mkuu wa Mambo ya Ufundi wa Kampuni ya Simu ya Zantel, Moncef Mettiji (wapili kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhiana mkataba wa maelewano ya kibiashara kati ya Taasisi zao. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Deos Mndeme.

Baadhi ya Maofisa wa Kampuni ya Simu ya Zantel, wakiwa katika hafla ya kukabidhiana mkataba wa maelewano ya kibiashara kati ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Kampuni yao hiyo, Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakiwa katika hafla hiyo.
Ofisa Uhusiano wa Shirika la Posta Tanzania  (TPC), Wilifred Miigo, akiwakaribisha wakuu wa Taasisi hizo pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya kukabidhiana mikataba ya maelewano ya kibiashara kati ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) na Kampuni ya Simu ya Zantel, ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam leo.(Picha zote na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad