Na Dotto Mwaibale wa Habari za Jamii Blog
SERIKALI imesema gharama za kutibu mgonjwa wa kisukari kwa mwaka hapa nchini ni sh.408,000 na kuwa watu wengi wamekuwa wakiugua ugonjwa huo bila ya wao kujitambua.
Imeelezwa kuwa utafiti uliofanya mwaka 2012 katika wilaya 50 nchini ulionyesha ya kuwa asilimia 9.1 ya watu huugua ugonjwa huo bila wenyewe kujua.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Naibu Waziri wa Afya Kebwe Stephen wakati akitoa tamko la serikali kuhusu siku ya ugonjwa huo ambayo itaadhimishwa duniani kote kesho alisema ugonjwa huo umekuwa na changamoto kubwa kwa vile hutokana na ulaji usiofaa.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa watoto wenye kisukari mwaka huu 2014 ni kati ya asilimia 15 mpaka 20 ya wagonjwa wote kisukari ambao wanatibiwa kwenye kliniki nchini.
"Maadhimisho ya siku ya kisukari yataadhimishwa katika hospitali zote za Rufaa, mikoa na ngazi za wilaya kwa wananchi wote kupima bure sanjari na kupata dawa,"alisema Kebwe.
Alisema watu wengine wanakuwa na dalili lakini huwa hawachukui hatua za mapema ili kuweza kuuzia ugonjwa huo kuendelea.
Alisema dalili za ugonjwa wa kisukari ni rahisi kuzitambua nazo ni kusikia njaa kila wakati,kukojoa mara kwa mara,kupungua uzito, na mwili kukosa nguvu.
Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Kisukari Duniani mwaka 2014 ni "Ulaji unaofaa, huanza na mlo wa asubuhi" na kuwa kauli mbiu hiyo inalenga kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya ulaji unaofaa ili kuepuka matatizo mbalimbali yanyotokana na ugonjwa wa kisukari katika jamii.

Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe Stephen (kulia), akizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo
mchana , wakati akitoa tamko la serikali kuhusu Siku ya Kisukari Duniani
itakayoadhimishwa duniani kesho.
Mkurugenzi
wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk.Ayoub Magimba (kulia), akizungumza
wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Kebwe
Stephen kuzungumza na wanahabari.
Kaimu
Mkurugenzi Msaidizi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Dk. Sijenunu
Aaron (kushoto) na Mratibu wa Kisukari wizarani hapo, Dk.Auson
Rwehumbize wakiwa kwenye mkutano huo.
"Hii
picha ni lazima niipate" ni kama anaongea Halima Kambi mpiga picha wa
Kampuni ya The Guardian Limited wakati Naibu Waziri Kebwe Stephen
alipokuwa akitoa tamko hilo kwa wanahabari.
No comments:
Post a Comment