Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani),kuhusiana na ujenzi wa mradi wa hospitali ya kisasa iliyopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zimetolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.
Kwa mujibu wa Profesa Shaban Mlacha kituo hicho ambacho kitajikita zaidi kwenye magonjwa ya figo kina maabara ya kisasa na vifaa vya kisasa huku kukiwa na vyumba 40 vya madaktari.
Taarifa ya mjenzi Habibu Nuru wa Hab Consult limited inayojenga kituo hicho amesema hadi sasa wamefikia asilimia 95 katika awamu ya kwanza na mradi ukimalizika utakuwa umetumia bilioni 36 za Kitanzania.
Fedha hizo zote zinatoka katika Mfuko wa Bima kwa lengo la kuhakikisha kuwa wanachama wake wanatibiwa vyema na wananchi wanapata huduma pia. Kituo hicho kitakuwa kinatibu magonjwa yote.
Profesa Shaban Mlacha akizungumza alisema kwamba kuwapo kwa kituo hicho na hospitali itakayojengwa itachangia si tu katika kufanya utafiti wa magonjwa na kutibia lakini pia itatoa nafasi kwa wanafunzi wa kitivo cha tiba UDOM na walimu wao kufanya mazoezi yanayostahili na kuonesha ubingwa wao. Jengo hilo lenye ghorofa tatu linaonekana kuwa moja ya kituo bora kabisa.
Jengo la hospitali ya kisasa lililopo ndani ya chuo cha UDOM kama lionekanavyo pichani ambalo ujenzi wake liko katika hatua za awali kukamilika,aidha kutokana na taarifa ya Kaimu Mkuu wa Chuo hicho cha Dodoma (UDOM),Prof.Shaaban Mlacha,amesema kuwa hospitali hiyo inatarajiwa kuanza kutoa huduma rasmi mnamo januari 2015 .Mradi huo umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36 zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.
Mshauri wa mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya UDOM,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa hospitali ya kisasa iliyopo ndani ya chuo hicho cha UDOM.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.
Pichani ni Mshaurii wa mradi wa ujenzi wa hospitali hiyo ya UDOM,kutoka kampuni ya HAB CONSULTANT,Bwa.Habib Nuru akifafanua jambo kwa baadhi ya Wanahabari ,kuhusiana na ujenzi wa mradi wa hospitali ya kisasa iliyopo ndani ya chuo hicho cha UDOM,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto.Mradi huo ambao unaelezwa kuwa umetumia kiasi cha fedha shilingi Bilioni 36,zilizotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF.
Pichani ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima (RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Pichani
ni Mganga Mkuu wa hospitali ya Singida,Dkt.Doroth Bwajima
(RMO),akizungumza mbele ya wanahabari na wadau wengine walioshiriki
kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa
Dodoma hotel mkoani Dodoma kuhusiana na mada yake iliyohusu Matumizi ya
Fedha za Uchangiaji (NHIF,CHF,PAPO KWA PAPO).kongamano hilo limeandaliwa
na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Pichani
ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo la siku mbili
linalofanyika mkoani Dodoma.
Pichani
ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kongamano hilo la siku mbili
linalofanyika mkoani Dodoma.
Wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zikijadiliwa ndani ya kongamano hilo mapema leo mchana.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti NHIF,Bwa.Raphael Mwamoto,Kaimu Mkurugenzi wa Tiba
na Ushauri wa NHIF,Bwa.Mkwabi Fikirini na Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF) wakiwa kwenye kongamano la tisa la Wanahabari linalofanyika kwenye moja ya ukumbi wa Dodoma hotel mkoani Dodoma mapema leo.
Pichani
ni baadhi ya Wadau mbalimbali na wanahabari wakifuatilia mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye kombano hilo la siku mbili
linalofanyika mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment