Tafrani kubwa imezuka jioni ya leo wakati wa Mdahalo wa kujadili umuhimu wa kuzingatia Mambo ya msingi katika katiba inayopendekezwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliokuwa ukifanyika kwenye Ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl, ubungo Plaza Jijini Dar es salaam.
Chanzo cha Tafrani hiyo,inaelezwa kuwa ni Baada ya Mh. Warioba katika taarifa yake kueleza kwamba Muungano sio tunu ila ni urithi ulioachwa na Waasisi,ndipo baadhi ya watu waliokuwepo kwenye Mdaharo huo wakahamaki na kuanza kuinua mabango yasemayo pamoja na mambo mengine kwamba iweje wajadili mapendekezo ya rasmi ya katiba ambayo wao wameshaikubali?
Likaanza zogo wati wengine wakijaribu kuwanyang'anya yale mabango na kuyachana ndipo vurugu/kashfa/matusi yakaanza kutolewa dhidi ya meza kuu. Hali hii ilisababisha kushikana, kusukumana na kurushiana viti.
Mdaharo huo ambao ulianza kufanyika katika Ukumbi huo kuanzia saa 9:20 alasiri ukiwa chini ya Uenyekiti wa Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba,ukiwa umeandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Mkutano ulihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali sambamba na itikadi tofauti za kisiasa. Mkutano ulirushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV kwa maudhui ya kimtazamo uliolenga kuoanisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya tume ya Warioba na ile ya Bunge Maalum la Katiba.
Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa kuondolewa kwenye Mdahalo huo mara baada ya kuzuka kwa tafrani hiyo.
Jaji Mstaafu Mh. Joseph Sinde Warioba akisaidiwa na Wanausama wa kuondolewa kwenye Mdahalo huo mara baada ya mambo kuharibika kutokana vurugu kubwa.
Ilikuwa ni tafrani tupu.
Hakuna Mdahalo tena.





No comments:
Post a Comment