Taasisi ya kijamii ya TWA (Tanzania Women of Achievement ) leo imezindua rasmi Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania ambazo zitafanyika Machi 7,2015 kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake ambao wamechangia maendeleo Tanzania katika nyanja tofauti.
Rais wa shirika la Wanawake Wenye Mafanikio Bi. Irene Kiwia alisema “ Lengo la TWAA ni kusheherekea mafanikio ya wanawake hawa na kazi wanazozifanya kwenye jamii kupitia nyanja tofauti ndani ya Tanzania. Vigezo mbalimbali vitatumika katika kuwachagua kama vile utofauti waliouonyesha katika jamii zao, jinsi gani wameweza kuwavutia na kuwashawahi watu wengine, na jinsi gani wameweza kuwagusa na kuwafikia watu tofauti tofauti."
Bi Kiwia alisema kwamba “ Tuzo hizi pia zitaenda sambamba na na mafunzo ya kujenga uwezo wa wasichana viongozi katika nyanja tofauti walio kati ya umri wa miaka 18-27 kutoka mikoa yote ya Tanzania ambayo yatachukua wiki 6. Wasichana hao watakutanishwa na wanawake wanaofanya vizuri katika biashara, kazi za jamii na idara tofauti kwa ajili ya kupewa motisha an kujifunza. Mategemeo yetu ni kuwa baada ya mafunzo haya wasichana wataenda kuwa chachu ya mabadiliko mikoani kwao na kuwafundisha wenzao wengi ili kusambaza mori wa maendeleo an mabadiliko kwa wasichana wadogo nchini kote.
Mwenyekiti wa TWAA, Mrs. Sadaka Gandhi alisema “suala la uwezeshaji kwa wanawake linapewa kipaumbele duniani kote, tuzo hizi zitaonyesha uwezo na ugunduzi wa wanawake katika sehemu tofauti. Tunaamini kuwa wale wote watakaoshiriki watakuwa chachu ya mabadiliko kwa wasichana kutoka vijijijini, wafanyabiashara na wanawake wengi chini Tanzania”.
"Katika kipindi cha miezi mitatu, tunaomba watu mbalimbali wajitokeze kuchagua wanawake ambao wanafanya vizuri katika fani zote kuanzia mfanyabishara mwenye jitihada kubwa, mwalimu wa namna ya kipekee na hata mtu ambaye ameweza kuleta mabadiliko muhimu katika jamii yake.” Alimalizia Mrs. Gandi.
Vipengele vya tuzo za mwaka huu ni sanaa na utamaduni, ujasiriamali, elimu, afya, sayansi na teknolojia, kilimo, ustawi wa jamii, michezo, umma, mshiriki wa mafanikio mwenye umri mdogo, mwanamke aliefanya vizuri ndani ya mwaka mzima na mwanamke aliefanya vizuri katika maisha yake.
Washiriki wanaweza kujipendekeza ama kupendekezwa la taasisi kupitia www.twa.or.tz, info@twaa.or.tz kabla ya tarehe 30 Januari 2015. Washiriki lazima wawe ni wakazi wa Tanzania ambao kazi zao zimefanyika Tanzania. Washiriki watatu katika kila kipengele watatangazwa kabla ya siku ya sherehe ya Tuzo za Wanawake Wenye Mafanikio mwezi Machi mwakani.
Kamati ya TWAA inawajumuisha Bi Mary Rusimbi - Mwanaharakati na Mwanzilishi wa Programu ya Mtandao wa Jinsia Tanzania, Jaji Joaquine De Mello, Dk. Marcelina Chijoriga - kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bwana. Innocent Mungy - Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), Sadaka Gandi - Mwanasaikolojia na mfanyakazi za Jamii, Irene Kiwia - Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya mahusiano ya jamii Frontline Porter Novelli.
Rais
wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania
Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia (kulia) akisisitiza jambo mbele
ya wanahabari (hawapo pichani) juu ya utoaji wa Tuzo za Wanawake wenye
Mafanikio Tanzania ambazo zitafanyika Machi 7,2015 kwa mara ya nne tangu
kuanzishwa kwake, ikiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake
ambao wamechangia maendeleo ya nchi katika nyanja tofauti.Wengine
pichani ni Mwenyekiti wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania
(TWAA), Mama Sadaka Gandhi (katikati) na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tuzo
za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia.
Mwenyekiti
wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA), Mama Sadaka Gandhi
(katikati) akitoa ufafanuzi juu ya namna Tuzo hizo zitakavyokuwa
zikitolewa na wanaohusika kupewa tuzo hizo,wakati wa mkutano na
wanahabari (hawapo pichani) uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya
Serena,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Taasisi ya kijamii
ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of
Achievement ),Bi. Irene Kiwia na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tuzo za
Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia.
Katibu
Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen
Kiwia akielezea namna ya wanawake watakavyoshiriki ili kuweza kupata
Tuzo hizo.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhulia Mkutano huo.
Timu
nzima ya Taasisi ya kijamii ya TWA (Tanzania Women of Achievement )
inayoratibu utoaji wa tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA)
wakiwa kwenye picha ya pamoja.






No comments:
Post a Comment