HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 17, 2014

KAIMU KATIBU TAWALA MKOA WA MBEYA CONSTANTINE MUSHI AFUNGUA RASMI SEMINA YA MAAFISA MAZINGIRA JIJINI MBEYA LEO

Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akitoa maelekezo kwa baadhi ya wawasilishaji mada katika mafunzo yanayoshirikisha maafisa mazingira katika mikoa ya Iringa na Mbeya yanayofanyika jijini Mbeya leo. Lengo la mafunzo hayo ni kuwashirikisha mpango kazi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na kupata michango yao. Kushoto ni Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Nyanda za Juu Kusini David Elias. Katikati ni Afisa Mazingira kutoka Wizara ya Nishati na Madini Abdullatif Nassor.
Afisa Misitu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Theodore Silinge akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege (kulia) akielezea shughuli za Kitengo chake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi ili aweze kufungua mafunzo hayo.
Sehemu ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa madini hotuba iliyokuwa inawasilishwa na mgeni rasmi Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi (hayupo pichani).
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi (katikati) akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Mbeya Constantine Mushi ( wa nne kutoka kushoto waliosimama mbele); Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Gideon Kasege ( wa tatu kutoka kushoto waliosimama mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad