HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 7, 2014

JK AOMBA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KUKABILI UJANGILI

GU9A8625
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha. (Picha zote na Zainul Mzige)

Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete ameitaka jumuiya ya kimataifa kushirikiana na Tanzania katika kukabiliana na majangili wanaomaliza tembo kwa lengo la kupata pembe zao.

Alisema kutokana na biashara nzuri ya pembe hiuzo duniani majangili wamekuwa na soko tayari kiasi cha kuendeleza vitendo vyao.

Alisema mitandao iliyopo inawezesha kuuawa kwa tembo hao na kufikishwa bidhaa za pembe katika soko haramu ambalo lipo duniani na hivyo bila ushirikiano wa kimataifa wanyama hao ambao ni urithi wa dunia watatoweka kabisa katika miaka ijayo.

Amesema takwimu zilizopo sasa nchini za tembo zinatisha.
Alisema mathalani kwa ujangili pekee kwenye mfumo wa ekolojia wa Selou-Mikumi tembo waliobaki ni 13,084 kwa mwaka jana kutoka Tembo 109,419 waliokuwepo mwaka 2006.
Alisema mfumo uliopo wa ujangili na soko la bidhaa hizo unafanya vita inayoendeshwa na Tanzania kuwa ngumu kama haitapata ushirikiano na mataifa mengine.

Alisema kutokana na ukweli huo wanataka mataifa jirani na jumuiya ya kimataifa kuingia katika mapambano ya kudhibiti biashara hiyo na hivyo kuwamaliza majangili na kuendelea kuhifadhi Tembo.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwenye ufunguzi wa mkutano mkubwa wa kudhibiti ujangili na hifadhi endelevu ya wanyamapori, alisema serikali ya Tanzania imeanzisha mchakato wa kulinda wanyama pori.
GU9A8723  
Baadhi ya wadau kutoka nchi mbalimbali wanaohudhiria mkutano huo akiwemo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad