HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 13, 2014

TASWIRA MBALI MBALI ZA MCHEZO WA VIONGOZI WA DINI ULIOCHEZWA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR

Mshambuliaji Machachari wa timu ya Mshikamano (kulia) akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya Amani katika Mchezo uliowakutananisha viongozi wa Dini nchini ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Amani na Mshikamano kwa Taifa la Tanzania uliocheza jana kwenye Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa Mchezo timu ya Amani ilishinda goli 1-0.Picha na Othman Michuzi.
Golikipa hodari kabisa wa timu ya Amani akidaka mpira kwa uhodari mkubwa katika Mchezo uliowakutananisha viongozi wa Dini nchini ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha Amani na Mshikamano kwa Taifa la Tanzania uliocheza jana kwenye Uwanja wa Taifa,jijini Dar es Salaam.hadi mwisho wa Mchezo timu ya Amani ilishinda goli 1-0.
Refarii wa kutumainiwa,Kamishna Suleiman Kova akiwa makini kabisa na mchezo huo.
Refarii akifatilia mpiria kwa makini....
Hayaaaa anakwenda Mshambuliaji wa Timu ya Mshikamano paleee..... anakwendaaaaa.... anaendelea kuichachafya ngome ya Amani.....
Anapiga shuti kali paleeeeeee.........Gooooo.... Daaaaahh.... hapana,ni Goooollll kikiiii.
Haya sasa ni Mapumzi na Walimu wanatoa Mawaidha wa wachezaji wao.
Mshika kibendera upande huu alikuwa ni AfandeValentino Mlowola kutoka Jijini Mwanza.
hasa sasa anakwenda paleeeee.....BOFYA READ MORE HAPO CHINI KUSHOTO KUONA PICHA ZAIDI

Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akikabidhi Kombe kwa kiongozi wa timu ya Amani,ambayo imeibuka kinara katika mashindano hayo kwa kuichapa timu ya Mshikamano goli moja.Mchezo huo wenye lengo la kuimarisha na kudumisha amani na mshikamano tulionao umefanyika katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar  ukijumuisha viongozi mbalimbali wa dini ya Kikristo na Kiislamu,ambapo pia viongozi wa ngazi mbalimbali wa dini na serikali walihudhuria.
 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikabidhi Kombe kwa kiongozi wa timu ya Mshikamano,ambapo timu hiyo imenyukwa goli moja dhidi ya timu ya Amani,mchezo huo wenye lengo la kuimarisha na kudumuisha amani na mshikamano tulionao umefanyika katika Uwanja wa Taifa,jijini Dar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali.
 Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Amani
 Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na timu ya Mshikamano
 Sehemu ya umati wa watu waliokuwepo kushuhudia mechi ya Amani na Mshikamano,iliyofayika jioni ya leo ndani ya uwanja wa Taifa.
 Waziri Mkuu Mh.Mizengo Pinda akizungumza jambo mbele ya wachezaji wa timu ya Amani na Mshikamano,zilizoundwa mahsusi katika kuadhimisha siku ya amani duniani,ambapo  viongozi wa dini uliojumuisha Masheikh, Maimamu, Maaskofu, Wachungaji na Mapadre.Mgeni rasmi katika mchezo huo alikuwa ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,Shoto kwake ni Mkuu wa  Mkoa wa Jiji la Dar,Mh.Said Meck Sadick na Rais wa TFF,Bwana Jamal Malinzi.

Katika mchezo huo wa kujenga amani na mshikamano uliopo nchini,Mwamuzi msaidizi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar,Mh. Said Meck Sadick na mwamuzi aliyeshika kipyenga alikuwa ni Kamishna wa Kanda Maalumu, Seleman Kova 
Mkuu wa Mkoa wa jiji la  Dar, Mh.Said Meck Sadick  ambaye alizungumza machache na kumkaribisha Mgeni Rasmi wa mchezo huo wa Viongozi wa Dini kati ya Amani na Mshikamano,Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda pichani kulia. 
 Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Mussa ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mchezo huo,akizungumza machache. 
 Rais wa TFF,Bwan, Jamal Malinzi akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa jiji la Dar, Mh.Said Meck Sadick  ambaye alizungumza macheche na kumkaribisha Mgeni Rasmi wa mchezo huo wa Viongozi wa Dini kati ya Amani na Mshikamano,Waziri Mkuu,Mh Mizengo Pinda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad