Wapenzi na mashabiki wa timu mbili za watani wa Jadi Yanga na Simba wakishiriki katika mchezo wa mpira wa meza wakati wa Uzinduzi wa Nani Mtani Jembe awamu ya pili kwenye viwanja vya Kiwanda cha TBL Jijini Mbeya.
Wafanyakazi
wa TBL jijini Mbeya wa ambao ni mashabiki wa Yanga na Simba
wakishindana kupiga danadana katika viwanja vya Kiwanda cha TBL Jijini
Mbeya.
Mashabiki
na wapenzi wa timu ya Simba ambao ni wafanyakazi wa TBL Mbeya
wakishangilia ushindi baada ya kuwashinda mashabiki na wapenzi wa timu
ya Yanga kwa upigaji wa danadana.
Wafanyakazi
wa TBL Mbeya ambao ni wapenzi na mashabiki wa timu za Yanga na Simba
wakichuana katika mchezo wa kuvutana kamba kwenye mashindano ya Nani
Mtani Jembe kwenye viwanja vya Kiwanda cha TBL.
Meneja
wa Bia ya kilimanjaro George Kavishe akielezea mpango wa awamu ya pili
wa Bia ya kilimanjaro katika utambulisho wa Nani Mtani Jembe ambayo
yanazihusisha timu mbili watani wa Jadi Yanga na Simba.
Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji wa timu ya Yanga Mohamed Bhinda akimkabidhi kadi
za uanachama Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Yohana Samwel kwenye mashindano
ya Nani Mtani Jembe kwenye viwanja vya Kiwanda cha TBL jijini Mbeya.
Mmoja
wa washiriki wa mashindano ya Nani Mtani Jembe mpenzi wa Simba kwa
upande wa wanawake akishiriki katika mashindano ya upigaji Danadana.
No comments:
Post a Comment