HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 13, 2014

MASHINDAO YA MADEREVA WA SCANIA YAMALIZIKA JIJINI DAR

Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano (kushoto) akimkabidhi kombe dereva Francis John Kinaulanga (kulia) baada ya kuibuka dereva bora wa mwaka 2014 wa shindano la scania ”Scania Driver of the year competition 2014” lililofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa shindano la Scania Scania Driver of the year competition 2014” Francis John Kinaulanga (katikati) akiwa na mshindi namba mbili Ramadhani Ahmad Danga (kulia) na Winston Rwegalulila Rwechungura (kushoto) baada ya kutangazwa washindi kwenye Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam.
Madereva wote wa shindano la scania ”Scania Driver of the year competition 2014” lililofanyika katika Viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akionyeshwa kitu kwenye kompyuta na Afisa mwendeshaji wa Scania,Kisali Nnyari.
Sehemu ya umati wa watu uliofika uwanjani hapo kujionea mashindano hayo.

DEREVA Francis John Kinaulanga ameibuka dereva bora wa mwaka 2014 wa shindano la scania ”Scania Driver of the year competition 2014” baada ya kuwabwaga wenzake saba.

Shindano hili ambalo lilivuta umati mkubwa wa watu japo kulikuwepo mvua za hapa na pale lilifanyika katika viwanja vya Tanganyika Parkers, Kawe jijini Dar es Salaam.

Nafasi ya pli ilichukuliwa na Ramadhani Ahmad Danga na nafasi ya tatu ilikwenda kwa Winston Rwegalulila Rwechungura ambao wote kwa pamoja walipata nafasi ya kwenda nchini Afrika Kusini kushiriki faibnali za Scania ambazo zitahusisha madereva wan chi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara.

Akizungumza wakati akikabidhi zawadi kwa washindi, Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano aliwapongeza madereva alishinda na kuwataka kuwa mfano bora kwa utii wa sheria barabarani.

“Nawapongeza madereva wote kwa kushiriki shindano hili lakini kipekee kwa washindi watatu wa mwanzoni na naowaomba muwe mabalozi wazuri wa utii wa sheria barabarani si kwamba muishie hapa kwenye shindano”, alisema Kahatano.

Pia aliipongeza kampuni ya Scania kwa kuendesha shindano hili kwani litaibua hari kwa madereva wengine kushiriki na kuwa chachu wa utii wa sheria za barabarani jambo ambalo litaepusha ajali za barabarani ambazo zinazepukika.

Naye Afisa mwendeshaji wa Scania Kisali Nnyari, alisema kuwa washndi watatu wa juu watagharamia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini wao na wenzao wao pamoja na bosi wa kampuni yake kwa siku saba kuanzia malazi, chakula na usafari wa kwenda na kurudi.

Shindano hili linafanyika kwa mara ya pili hapa nchini na limeacha gumzo kwa watu waliojitokeza kushuhudia huku madereva wengine wakiomba kuingizwa kwenye orodha ya washiriki bila kupitia hatua za awali jambo ambalo lilishindikana kukutokna na sheria za shindano lenyewe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad