HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 13, 2014

KLABU YA MICHEZO YA GST LEO YAKABIDHI KOMBE BAADA YA SHIMIWI KUMALIZIKA

Klabu ya michezo ya Wakala wa Jiolojia Tanzania, yafanya vizuri katika mashindano ya Shirikisho la michezo ya Wizara , Idara na taasisi za serikali (SHIMIWI) yaliyofanyika mkoani Morogoro kwa mwaka 2014.

Katika mashindano hayo klabu ya GST iliweza kupeleka wanamichezo katika mchezo wa mpira wa pete , kuvuta kamba , riadha , mbio za baiskeli , draft , dasti na mchezo wa bao , katika michezo hiyo GST imeweza kupata medali mbili za shaba kutoka mchezo wa mbio za mita 100 , kombe moja kutoka mchezo wa draft.

Kaimu Mtendaji Mkuu , Bi Augustine Rutaihwa akizungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu katika makabidhiano ya kombe hilo ndani ya viwanja vya GST, aliwahimiza wanamichezo kushiriki michezo na kufanya mazoezi pale wanapopata muda kwa manufaa ya afya ya akili na mwili .

Kwa upande wake katibu mkuu wa klabu ya michezo ya GST , Bw Heri Issa Gombera , alimuomba Mtendaji Mkuu ambaye ndiye mdhamini wa klabu juu ya ushiriki wa michezo ya bonanza la michezo kwa watumishi kwa lengo la kuimarisha mahusianao baina ya watumishi na ofisi.

Klabu ya michezo ya GST ilianza kushiriki mashindano ya SHIMIWI mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad