HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 8, 2014

ZIMWI LA AJALI LAZIDI KUIMALIZA TANZANIA,NYINGINE YATOKEA MCHANA HUU ENEO LA GAIRO NA KUPOTEZA MAISHA YA ZAIDI YA WATU WANNE

Ajali nyingine mbaya:Basi la Abiria linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam - Tabora limepata ajali mbaya sana mchana huu katika eneo la  Kiegeya,Gairo na kupelekea zaidi ya watu wanne kupoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.Ni majonzi makubwa yametawala katika eneo hilo hivi sasa,huku juhudi za kuokoa miili na majeruhi zikiendelea kama inavyoonekana pichani.ni siku tatu tu zimepita toka ajali nyingine mbaya itokee huko Musoma na kupoteza maisha ya zaidi ya Watanzania 35.Ripota wa Globu ya jamii yupo eneo la tukio hivi sasa na taarifa kamili itawajia baadae kidogo.


Basi la Kampuni ya Air Bus likiwa halitamaniki baada ya kupata ajali mchana wa leo katika eneo la Kiegeya,Gairo na kupelekea zaidi ya watu wanne kupoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.

1 comment:

  1. Inasiktisha sana tena sana . Mie najiuliza kwanini serikali haiweki sheria na kuzisimamia. Angalia nchi za europe ukipata ajali kizembe unafutiwa kuendesha gari . huku ukiingia shule ya udereva unafundiswa hata na baba yako lakini siku ya kupat driving les..yako lazima uende kwa waliosajiliwa na serekali. ukikutwa umekunywa bia moja hurusiwi kuendesha gari mwaka.. Sasa hizi ajali mpaka linina mpaka lini tumsingizie Mungu jamani!!!!

    ReplyDelete

Post Bottom Ad