Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kabla ya kukabidhi mabasi 6 kwa wakuu wa vyuo vya Afya kutoka katika maeneo mbalimbali .Mabasi hayo yatasaidia kuaondoa upotevu wa muda na adha ya usafiri waliyokuwa wakiipata wanafunzi,watumishi na wakufunzi wa vyuo hivyo kufika kwenye maeneo ya mafunzo kwa vitendo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akikata utepe kwenye basi moja kati ya sita yaliyonunuliwa kwa ufadhili wa Mradi wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambayo yamekabidhiwa kwa wakuu wa vyuo vya afya leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Charles Pallangyo akikagua mabasi hayo yaliyonunuliwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia mzunguko wa 9 ambayo yamekabidhiwa kwa wakuu wa vyuo 6 vya afya leo jijini Dar es salaam.
Sehemu ya ndani ya mabasi hayo yaliyotolewa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mradi wa Mfuko wa Dunia. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.
No comments:
Post a Comment