HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 20, 2014

WANACHAMA WAIOMBA BIMA YA AFYA KUGHARAMIA KIPIMO CHA VINA SABA (DNA)

BAADHI ya wanachama wa mfuko wa Bima ya afya (NHIF) wameutaka mfuko huo kugharamia kipimo cha vina saba (DNA) kwa wananchama wake pamoja na gharama za nauli na posho kwa wanachama wanaokwenda kupata matibabu nje ya vituo vyao vya kazi.

Wanachama hao waliyasema hayo katika kijiji cha Mwamgongo wakati wa kikao cha pamoja baina ya wanachama hao na uongozi wa mfuko wa Bima ya afya(NHIF) Mkoa wa Kigoma.

Nassib Ally mtumishi wa afya katika kituo cha mwamgongo alisema kuwa pamoja na kwamba malipo ya posho na nauli kwasasa ya kwenda kutibiwa nje ya kituo hulipwa na mwajiri lakini malipo hayo hayalipwi kwa wakati.

Alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwafanya wanachama kuhangaika wanapofuatilia matibabu nje ya vituo vyao vya kazi.

Naye Mussa mwalimu wa shule ya Msingi Nyambusho iliyopo kijijini hapo alisema kuwa aliutaka mfuko kugharamia upimaji wa vinasaba(DNA)pamoja na kugharamia matibabu ya nje ya nchi kwa wananchama wake.

Akijibu juu ya maombi hayo Meneja wa Bima ya afya Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo alisema kuwa kwasasa mfuko wa Bima ya afya haugharamii malipo ya posho na nauli kwa wanachama wake wanaopata rufaa ya matibabu nje ya vituo vyao vya kazi,Alisema suala hilo linabaki kuwa la muajiri.

Odhiambo alisema pia suala la kugharamia matibabu nje ya nchi litabaki suala la Wizara ya afya na huku suala la upimaji wa vinasaba likibaki kuwa la gharama za mtu binafsi.
Mkuu wa kituo cha afya Mwamgongo Dkt Swagala akipokea msaada wa mashuka 50 toka kwa meneja wa Bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kigoma Elias Odhiambo.
Meneja wa mfuko wa Bima ya afya (NHIF)Mkoa waKigoma Elias Odhiambo akikabidhi moja ya mashuka 50 kwa uongozi wa Kituo cha afya cha Mwamgongo kilichopo mwambao wa kaskazini mwa Ziwa Tanganyika Wilaya ya Kigoma.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha mwamgongo waliojitokeza kupima afya zao katika shule ya msingi mwamgongo zoezi lililokuwa likiratibiwa na mfuko wa Bima ya afya(NHIF) Mkoa wa Kigoma.Picha zote na Editha Karlo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad