Rais wa Uganda Yoweri Museveni akiteremka
katika ndege iliyomleta leo jijini dar es Salaam kwa ajili ya ziara yake ya siku moja nchini Tanzania .
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Kikwete akikagua Gwaride la Maaskari pamoja na Mgeni wake Rais wa
Uganda Yoweri Museveni baada ya kuwasili leo jijini katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu
Julius Nyerere kwa ajili ya ziara ya siku moja.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete (Kulia) pamoja na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni (kushoto) wakiangalia
ngoma za utamaduni baada ya kuwasili katika
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu
Julius Nyerere Leo jijini Dar es Salaam
,kwa ajili ya ziara ya siku moja hapa nchini.
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete (Katikati)akipata maelekezo kutoka kwa mwongoza msafara na
kushoto ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni ambaye amewasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya siku moja . ( Picha na
Lorietha Laurence-Maelezo).
Ndege iliyomleta Rais wa Uganda Yoweri
Museveni ikiwa imetua katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa ziara yake
ya kikazi ya siku moja ambapo alipokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment