Msajili wa Bodi, Jehad A. Jehad (kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani, Ezekiel Stephen na Kaimu Nsajili Msaidizi Ufundi, Mashaka Bundala.
Kikao na waandishi wa habari kikiendelea.
Na Dotto Mwaibale
BODI
ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) katika
kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi sasa imezifungia kampuni 36 na wakandarasi 86 kufanyakazi ya ukandarasi baada ya kushindwa kufuata sheria za ujenzi.
Hayo
yalielezwa na Msajili wa bodi hiyo Jehad Jehad wakati akizungumza na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa usajili wa
wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi utakaofanyika ukumbi wa mikutano
wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Septemba 18, 2014 jijini Dar es
Salaam.
"Kazi
yetu kubwa ni kusimamia sheria ya shughuli za ujenzi na kama tukibaini
kuna kampuni inakwenda kinyume tunaifungia kufanyakazi" alisema Jehad.
Alisema
lengo mkutano huo wa Septemba 18 ni kuwanoa wataalamu wa fani hiyo ili
kukabiliana na mabadiliko ya kiteknologia na kitaaluma katika sekta ya
ujenzi, kubadilishana mawazo na kuboresha huduma za taaluma hiyo.
Akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali Mwenyekiti wa bodi hiyo Dk.Ambwene
Mwakyusa alisema Tanzania haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi
kwa ujumla (Building Codes) itakayoweza kuwabana wajenzi ya maghorofa
ambayo yanabomoka hapa nchini. Dk. Mwakyusa alisema sheria hiyo
ingekuwepo ingewaongoza wataalamu wa majengo jinsi ya kutumia vifaa vya ujenzi kwenye jengo husika tofauti na ilivyosasa.
Dk.Mwakyusa
alisema kutokana na sheria hiyo kutokuwepo wataalamu wa majengo
wanapotumia vifaa vya ujenzi ambavyo havina kiwango na wanapofikishwa
kwenye vyombo vya sheria baada ya majengo wanayojenga kuanguka wanakutwa
hawana hatia.
“Tanzania
haina sheria inayoratibu shughuli za ujenzi kwa ujumla kama ikiwepo
sheria itamuongoza mtaalamu wa majengo afuate sheria iliyopo jinsi ya
kutumia vifaa vya ujenzi mfano kama mbao au nondo zinatakiwa zitumike
aina gani kwenye jengo husika ,”alisema Dk.Mwakyusa. Katika mkutano huo
mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Hassan
Mwinyi.
No comments:
Post a Comment