Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Watendaji mbalimbali hawapo pichani kutoka, Wizara ya Ujenzi, TEMESA na Kikosi cha Maji cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamefanya kazi kubwa ya ukarabati wa Kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akipanda ngazi kwenda kukagua Kivuko cha MV Kigamboni ambacho matengenezo yake makubwa yanakamilika leo.
Luteni Kanali Gwanafi kulia akimuongoza Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwenda kukagua Kivuko cha MV Kigamboni sehemu ya chini mara baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.
Luteni Kanali Gwanafi wapili kutoka kulia akitoa maelezo kuhusu ukarabati mkubwa wa Kivuko cha MV Kigamboni kama inavyoonekana.
Taswira-Kivuko cha MV Kigamboni kinavyoonekana mara baada ya Ukarabati wake.
Luteni Kanali Gwanafi kulia akimuonesha Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli sehemu ya juu ya Kivuko cha MV Kigamboni.
Luteni Kanali Gwanafi kushoto akimuonyesha Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kuhusu sehemu ya chini ilivyokarabatiwa.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha MV Kigamboni huku akipatiwa maelezo kuhusu ukarabati wake.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza kwa makini Luteni Kanali Gwanafi kuhusu mambo mbalimbali wanayofanya ndani ya kivuko cha MV Kigamboni.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoka ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni mara baada ya ukaguzi wake. Picha zote kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi
No comments:
Post a Comment