HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 3, 2014

FILAMU YA ‘MATESO YA UGHAIBUNI’ KUZINDULIWA JIJINI DAR

Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, (Wa pili toka Kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni inayotarajiwa kuzinduliwa siku ya Alhamis Septemba 4, 2014 katika viwanja vya Leadrs Club. Pembeni yake ni Rais Wa Bongo Movie Steve Nyerere na wasanii wengine.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
FILAMU ya ‘Mateso Ughaibuni’ ambayo imerekodiwa Uingereza na wasanii Issa Musa ‘Cloud 112’, Riyama Ally, Wastara Juma na Monalisa itazinduliwa Alhamisi hii katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif, ambaye kampuni yake ndiyo iliwapeleka wasanii hao Uingereza kwenda kurekodi filamu hiyo, alisema licha ya kampuni yake kujihusisha na mambo ya mavazi na vitu vingine ameona kuna kila sababu ya kuwasaidia Watanzania wanaofanya sanaa ya uigizaji.
Rais wa Bongo Movie Steve Nyerere akiongea machache mbele ya waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa Filamu ya Mateso Ughaibuni. Pembeni yake ni Mkurugenzi wa Didas Fashion, Khadija Ayoub Seif na Flora Mvungi.

Waandishi wa Habari wakifuatilia kwa makini.
Wafanyakazi wa PSPF nao walikuwepo kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

1 comment:

  1. JAMANI FILM HII TUSIIKOSE YANAYOONGELEWA JAPO NIMEISIKILIZA SPORA SHOW NA NIMEONA TRELA NAAMINI ITAKUWA BOMBA. NA NI KWELI TUKIJA ULAYA BAADHI YA WASO NA NDUGU HUTESEKA , MTANZANIA MWENZIO HUCHUKUA KIGEZO KUKUNYANYASA TENA UKILETA MDOMO ANAKWAMBIA NIPIGE SIMU UNAISH BILA KIPANDE ???
    TUIGE MFANO WASOMALI,WAARABU NA MATAIFA MENGINE WANASHIKAMANA ,WANABEBANA ,SIE HATUNA UMOJA WETU NA TUKIWA NAO UKIINGIA TU ,LOOO KAOLEWA NA MZEE ,LOO HAVAI ,LOO ANARINGA ,LOO ACHANENI NAEV
    JE TUTATENGANA MPAKA LINI ???
    TUNAISHI TUKIOGOPANA KAA WANYAMA !!!
    TUNAISHI TUKIWEKEANA CHUKI KAA WAPALESTINA NA WAISRAELI!!!
    SASA TUFUNGUE MACHO TUJIPANGE UPYA
    AKIPATA MWENZIO WEWE PANGA FOLENI NYUMA AKE ZAMUYAKO ITAFIKA

    ReplyDelete

Post Bottom Ad