Vijana wawili wamechomwa moto katika eneo la Tabata Liwiti wakituhumiwa kuiba
pochi ya mwanamke katika eneo hilo,Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa
lilitokea asubuhi ya jana (Jumamosi)
ambapo walikuwa watatu wakafukuzwa na
watu mbalimbali.
Alisema kuwa walipokamatwa walipigwa na
kisha kuchomwa moto.
"Matukio haya yamekuwa yakitokea
mara kwa mara hapa Tabata na wezi
wanaoiba kwa kutumia pikipiki wamekuwa
ni kero kubwa sasa na kila wakikamatwa
na kupelekwa vituoni wanaachiwa na Polisi ila kwa sasa wananchi
wameamua kutumia sheria mkononi."
Askari kanzu wa Jeshi la Polisi wakipakia kwenye gari mabaki ya miili ya vijana wawili waliotuhumiwa kuwa ni wahalifu wa uwizi waliochomomwa moto jana maeneo ya Tabata Liwiti,jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wananchi wakazi wa Tabata Liwiti pamoja na Askari Kanzu wa Jeshi la Polisi wakiangalia mabaki ya miili ya vijana wawili waliosadikiwa kuwa ni wahalifu wa uwizi waliochomomwa moto jioni maeneo ya Tabata Liwiti,jijini Dar es salaam.
Hii ndio pikipiki waliokuwa wakiitumia wahalifu hao.
Picha na Evance Ng'ingo wa
habari5blog
No comments:
Post a Comment