Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiongea na waandishi wa habari eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati wa kupokea na kukabidhi vifaa vya kupima dalili za ugonjwa wa Ebola. Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Dharula na Maafa (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifani.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kebwe Steven Kebwe akiangalia kwa karibu taarifa zilizorekodiwa na moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Steven Kebwe (kulia)
akimkabidhi Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya
na Ustawi Dkt. Elias Chinamo moja ya kifaa (kamera) itakayotumika kupima
dalili za ugonjwa wa Ebola kwa wasafiri wanaoingia nchini kupitia
viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama kwa
kuuzuia ugonjwa huo kuingia nchini.
Mkurugenzi wa Ugavi wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD),Heri Mchunga (kushoto) akimpima
Mkurugenzi wa Afya na Usafi wa Mazingira wa Wizara ya Afya na Ustawi
Dkt. Elias Chinamo (kulia) kuonyesha namna moja ya kifaa cha kupimia
joto la mwili wa Binadamu kinavyofanya kazi kwa kubaini dalili za
Ugonjwa wa Ebola eneo la uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam.
Moja ya kifaa (kamera) nne zilizoagizwa na Serikali kupimia dalili za ugonjwa wa Ebola maeneo ya viwanja vya ndege. Kifaa hicho
kina uwezo wa kutunza picha na kumbukumbu za msafiri, muda , joto la
msafiri, tarehe aliyoingia nchini pia uwezo wa kupata takwimu kutoka
kwenye hali ya majimaji au jasho la Binadamu pindi kinapoelekezwa kwake.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
No comments:
Post a Comment