Kameraman wa Mtaa kwa Mtaa Blog jijini Mbeya,alifanya ziara fupi katika baadhi ya maeneo ndani ya Jiji hilo na kubaini maeneo mengi ya mji huo yakiwa ni machafu kupindukia,hii inatokana na baadhi ya wakazi wenyewe kwenye maeneo hayo kutokujali hali ya mazingira yanayowazunguka kwa hupenda kutupa uchafu hovyo hovyo bila hata ya kujali kwamba hali hiyo,inaweza kuwaletea matatizo ya kiafya wao wenyewe na faminia zao.
Ukiangalia kwa makini ndani ya mtaro huu utabaini ni kitu gani ninachokizungumzia hapa,kwani mtaro huo umekithiri uchafu kana kwamba hilo ndilo dampo kuu kwa eneo lote la hapo.
Watoto nao hawana nongwa,kwani michezo kwao ni wajibu.lakini kwakuwa hawana pa kwenda hivyo wamelazimika kupiga kambi pembeni ya mtaro wa maji machafu huku wakiendelea na yao.
na mtaro huo ni kama unavyoonekana.
na mtaro huo ni kama unavyoonekana.
Uchafu umeshakuwa sugu huu.....
Madogo waleee wakipiga misele.. Utawataka sasa...
Kiukweli hali si hali katika maeneo mengi ya jiji hili.Picha zote na Fadhil Atick wa Mtaa kwa Mtaa Blog,Mbeya.
No comments:
Post a Comment