HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 16, 2014

Moto wateketeza kituo cha kupozea umeme cha mjini Moshi leo asubuhi

Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini. 
Transforma zinazosambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi Mkoani Kilimanjaro zilizoko eneo la Bomambuzi zimewaka moto asubuhi hii muda mfupi baada ya kutokea shoti ambayo haijafahamika chanzo chake ni nini. 

 Moto huo umetokea majira ya saa 1:10 na kusababisha maeneo kadhaa ya mji wa Moshi kukosa umeme hadi sasa. 
 Globu ya jamii imeshuhudia kikosi cha zimamoto kutoka manispaa ya moshi kikijaribu kuzima moto huo ambao hata hivyo ulikwisha teketeza sehemu kubwa ya  kituo hicho cha kupozea umeme.
Askari wa kikosi cha Zimamoto wakifika eneo la tukio asubuhi hii
Wananchi wakishuhudia juhudi za kuzima moto huo
Moto ukiendelea 
Juhudi zikiendelea. Picha na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad