HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 12, 2014

MAMA TUNU PINDA ASHIRIKI MKUTANO WA AMANI NA USALAMA DUNIANI,UNAOFANYIKA NCHINI KOREA KUSINI

Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akifuatilia matukio kwenye ukumbi wa Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini. Wa pili kulia ni Rais mstaafu wa Mali, Prof. Dioncounda Traore. Wa kwanza kushoto ni Rais wa Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese na mkewe Bibi Filifilia Tamasese.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na Rais wa Samoa, Bw. Tui Atua Tupua Tamasese (kulia) na mkewe Bibi Filifilia Tamasese (Agosti 12, 2014). Wa pili kushoto ni Katibu Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad ambao wameandaa mkutano huo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Universal Peace Federation (UPF), Bw. Tageldin Hamad (kushoto) ambao wameandaa mkutano huo. Kulia ni Dk. Amalberga Kasangala kutoka Tanzania ambaye pia anashiriki mkutano huo.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na Rais wa Universal Peace Federation (UPF), Dk. Thomas Walsh (kushoto) na wajumbe wengine wanaoshiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwa na wajumbe wengine kutoka Afrika Kusini, Japan na Marekani ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini.
Baadhi ya wajumbe kutoka Kenya, Tanzania na Lesotho ambao wanashiriki Mkutano wa Dunia kuhusu Amani na Usalama unaoendelea jijini Seoul, Korea Kusini. (PICHA NA IRENE BWIRE WA OWM).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad