Meneja wa Castle Lager, Kabula Nshimo akitangaza fainali za mashindano ya Castle Lager Perfect Six ambayo yatafanyika Jumamosi jijini Dar es salaam.
Mashindano ya Castle Lager Perfect 6 ambayo yalifanyika nchi nzima katika muda wa miezi
mitatu yatafikia tamati wikendi hii katika fainali ambazo zitachezwa kwenye viwanja vya
Leaders jijini Dar es salaam tarehe 16 Agosti, 2014 ambapo kiingilio itakuwa ni bure. Washindi
wa fainali hizo zinazosubiriwa kwa hamu watatembelea uwanja wa Camp Nou na kuishuhudia
timu ya FC Barcelona ikicheza laivu na safari hiyo itagharamiwa kila kitu na Castle Lager.
Meneja wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo amesema leo kwamba Fainali za Castle Lager
Perfect 6 zitahusisha timu nane ambazo zilishindana kwenye kanda sita za nchi wakati wa
mashindano hayo ikiwemo timu ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA).
“Timu zitakazoshiriki kwenye fainali za Castle Lager Perfect 6 ni pamoja na Pile United
(Temeke), Barafu FC (Ilala), Infinity Communications (Kinondoni), Musoma Veterans (Musoma),
Kitayosa FC (Arusha), Schalke 04 (Morogoro), Green City (Mbeya), na TASWA FC (Vyombo vya
Habari).”
Nshimo alisema “Timu itakayoshinda fainali hizo itakuwa pia imeshinda nafasi ya aina yake
kwenda Hispania kutembelea uwanja mkubwa zaidi barani Ulaya wa Camp Nou unaomilikiwa
na FC Barcelona. Timu hiyo itaweza kujionea vivutio mbalimbali huko Camp Nou na kuishuhudia
FC Barcelona ikicheza mechi laivu kwenye uwanja huo maarufu.”
Nshimo aliongeza kuwa mambo yote yatakuwa Leaders Club wikendi hii ambapo fainali hizo
zitasindikizwa na burudani kabambe kutoka kwa msanii maarufu wa muziki wa dansi Ali
Choki mbaye ni kati ya waimbaji bora nchini pamoja na bendi yake ya Extra Bongo. “Ali Choki
ataburudisha wachezaji pamoja na watazamaji kwa nyimbo zake mbalimbali zinazopendwa
katika tukio hili ambalo linatarajiwa kuwa na msisimko mkubwa.” Ili kuhakikisha wachezaji
na mashabiki wanaburudika kutakuwepo na viburudisho na Nyama Choma wakati michezo
ikiendelea.
Pia Nshimo alisema kwamba, droo kubwa ya kampeni ya SMS ya iliyoenda sambamba
na mashindano ya Castle Lager Perfect 6 itafanyika siku hiyo na kupata washindi ambao
wataandamana na timu itakayoshinda kwenda Camp Nou.
Mashindano ya Castle Lager Perfect 6 Tournament yalizinduliwa mwezi Aprili mwaka huu Six
yakiwa yamelenga kuzungumza na wanywaji wa Castle Lager ambao wana shauku ya kucheza
mpira wa miguu, kuleta pamoja wanywaji wa Castle Lager ili wafurahie pamoja na kuwapa
zawadi wateja wa bia hiyo.

.jpg)
No comments:
Post a Comment